IQNA

Algeria mwenyeji wa mashindano ya Qur'ani

19:08 - June 16, 2012
Habari ID: 2347946
Duru ya tisa ya mashindano ya kimataifa ya tafsiri na kiraa ya Qur'ani Tukufu imepangwa kufanyika katika mtaa wa Dar al-Imam katika mji mkuu wa Algeria, Algiers tokea tarehe 8 hadi 14 Agosti.
Mashindano hayo ambayo yatawashirikisha vijana walio na umri wa chini ya miaka 25 yatafanyika kwa usimamizi wa Rais Abdul Aziz Bouteflika wa nchi hiyo.
Waziri wa Masuala ya Dini na Wakfu wa nchi hiyo ametoa taarifa akisema kuwa mashindano hayo ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani hufanyika kila mwaka na kwa usimamizi wa rais wa nchi hiyo. Washindi wa mashindano hayo hutunukiwa zawadi katika siku za sherehe ya Idul Fitr ambapo viongozi wa serikali na mabalozi wa nchi za Kiislamui pamoja na wanazuoni wa nchi hiyo hushiriki.
Waziri huyo ameongeza kuwa kuna mipango mingine ya kuandaa mashindano ya kimataifa kama hayo kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 15. 1030628
captcha