IQNA

Qur'ani ya kwanza iliyoandikwa kwenye jiwe kuonyeshwa

19:22 - June 16, 2012
Habari ID: 2347948
Qur'ani ya kwanza iliyoandikwa kwenye jiwe duniani ambayo imeandikwa na msanii wa Iran ambaye ni mlemavu wa vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran, itaonyeshwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Msanii huyo ameandika Qur'ani hiyo kwa muda wa miezi 31. Kwa mujibu wa tovuti ya CHIN msanii huyo Sayyid Hussein Pur Ridhawi amesema maandishi madogo ya Qur'ani hiyo yanaweza kusomeka bila kutumika chombo cha kukuza herufi.
Mwanasanaa huyo ameandika aya kama vile ya Kursi na baadhi ya dua mashuhuri za Kiislamu kwenye mawe yaliyo na udogo wa sentimita 10 na kuyaweka kwenye fremu maalumu. Amesema amechukua hatua za lazima kwa ajili ya kusajiliwa sanaa hiyo kwa jina lake katika taasisi husika kitaifa na kimataifa.
Msanii huyo tayari huko nyuma ameshaandika juzuu moja ya Qur'ani kwenye tawi la mti na anasema anakusudia katika siku zijazo kuandika Qur'ani nzima kwenye tawi la mti. 1030672
captcha