Katika safari yake ya hivi karibuni huko Kabul mji mkuu wa Afghanistan, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ametembelea na kushuhudia kwa karibu Qur'ani kubwa zaidi duniani inayoonyeshwa katika Kituo cha Utamaduni cha Hakim Nasr Khosro Balkhi mjini humo.
Bwana Ihsanoglu ambaye aliwasili mjini Kabul tarehe 14 Juni kwa lengo la kushiriki kwenye kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zonazopakana na Afghanistan na kieneo, amesema alipoonana na Mansur Nadi aliyetoa fikra ya kuandikwa Qur'ani hiyo kwamba, Qur'ani hiyo ni matunda muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu ambayo yanapaswa kuarifishwa kwa walimwengu. Qur'ani hiyo iliyoandikwa na Muhammad Sabir Husseini, mwanakaligrafia mashuhuri wa Afghanistan, kwenye kurasa 218 zenye ukubwa wa sentimita 228x155, imeandikwa kwa muda wa miaka mitano. 1030704