IQNA

Iran kuwaenzi wanawake wanaharakati wa Qur’ani

16:37 - June 17, 2012
Habari ID: 2348359
Kongamano la tatu la kuwaenzi wanawake wanaharakati katika masuala ya Qur’ani Tukufu litafanyika Juni 30 pembizoni mwa Mashindano ya 29 ya Qur’ani Tukufu ya Iran mjini Tehran.
Katibu wa kongamano hilo Bi Maasouma Farzanah amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa wanawake 29 wataenziwa katika kongamano hilo ambalo litafanyika katika Mnara wa Milad.
Amesema waliofuzu wanajishughulisha na masuala ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani, kufundisha Qur’ani, sanaa ya Qur’ani, utafiti wa Qur’ani n.k.
Bi. Farzaneh amesema kuwa katika makongamano mawili yaliyopita, mashirika na taasisi za Qur’ani zilitakiwa kupendekeza wanawake bora katika shughuli za Qur’ani lakini mwaka huu wanaharakati wa Qur’ani wametakiwa wajaze fomu katika tovuti ya www.awqaf.ir ili kujiarifisha.
Wawakilishi wa nchi 65 kutoka nchi za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu watashiriki katika awamu ya 29 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran.
Mashindano hayo yataanza Jumatatu Juni 18 sambamba na sherehe za Mab'ath ambazo hufanyika 27 Rajab na kuendelea hadi Juni 23 .
1029074
captcha