Warsha hiyo ambayo imehudhuriwa na walimu wa masomo ya dini imehutubiwa na mhadhiri wa elimu za dini katika Chuo Kikuu cha Bolu İzzet Baysal Mustafa Uonadr ambaye amesema kuwa idadi ya washiriki imeongeza sana mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita kutokana na kuondolewa kizuizi cha umri.
kabla ya kuanza warsha hiyo Sheikh Ömer Faruk Bilgili ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa mji wa fathiyye nchini Uturuki amesema kuwa kwa mujibu wa ratiba ya kila mwaka jumuiya ya masuala ya kidini ya Uturuki huanzisha masomo ya dini kwa ajili ya wananchi wa rika na umri tofauti, kwa msingi huo kufanyika warsha hiyo kwa ajili ya walimu kunawapa fursa ya kujiimarisha na kujitayarisdha vyema zaidi kwa ajili ya kutoa mafunzo na elimu. 1032051