IQNA

Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaanza mjini Tehran

10:08 - June 18, 2012
Habari ID: 2349084
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza Jumapili hapa mjini Tehran yakishirikisha mahafidh na maqari kutoka karibu nchi 70 za mabara matano ya dunia.
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza Jumapili hapa mjini Tehran yakishirikisha mahufadh na maquraa kutoka nchi 70 za mabara matano ya dunia.
Mkuu wa ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo kuwa, karibuni hivi mwamko wa Kiislamu utaenea katika kila pembe ya dunia.
Mwandishi wa Radio Tehran amemnukuu Hujatul Islam Walmuslimin Muhammad Muhammadi Golpayegani akisema hayo na kuongeza kuwa, mapinduzi ya wananchi yaliyopelekea kupinduliwa tawala kadhaa za kidikteta katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ukiwemo utawala wa dikteta Hosni Mubarak wa Misri ni ushahidi wa wazi wa kuenea mwamko wa Kiislamu katika nchi za eneo hili.
Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza 27 Rajab kwa munasaba wa kukumbuka kubaathiwa Mtume Muhammad SAW sawia na Juni 17 yanatarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa ya tarehe 22 Juni.
Mahafidhi 47 na maqarii 56 kutoka kona mbalimbali za dunia wanachuana katika mashindano hayo.
1032395
captcha