Siku ya Jumapili viongozi wa Jumuiya ya Mafunzo ya Qur'ani Tukufu katika mkoa wa Hadhramaut walikutana na kujadili suala hilo na Ahmad Mahfudh bin Zeidan, Mkurugenzi Mkuu wa Idhaa ya Sayoun ya Yemen. Pande mbili zimekubaliana jinsi mashindano hayo yaliyopewa jina la Warattil al-Qur'an yatakavyokuwa yakipeperushwa hewani kupitia redio hiyo.
Mashindano hayo ambayo hufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani yamekuwa yakifanyika kwa muda wa miaka 17 sasa.
Akizungumza katika kikao hicho, Omar Awadh Mazru' Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mafunzo ya Qur'ani Tukufu amesema kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuimarisha mashindano hayo, kupokea mapendekezo na kushirikiana na taasisi nyinginezo za Qur'ani.
Katibu Mkuu wa Redio Sayoun naye amesema kuwa redio hiyo iko tayari kushirikiana na pande husika kwa madhumuni ya kuimarisha kiwango cha mashindano hayo. 1033163