Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kielimu ya Kuhudumia Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw). Mashindano hayo yanahesabiwa kuwa ya kwanza ambayo yanadhaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu.
Jumuiya ya Qur'ani ya Maadh imetoa taarifa ikisema kuwa mashindano hayo ndiyo makubwa zaidi nchini Yemen ambayo hadi sasa yamewashirikisha mahafidh 95000 walioshiriki katika mashindano mengine madogo 6330. Jumuiya hiyo ya Qur'ani imesema washiriki wa mashindano hayo watajumuishwa katika makundi sita ya hifdhi ya juzuu 10 za Qur'ani, juzuu 20 sambamba na hifdhi ya Tuhfatul Atfaal, hifdhi ya Qur'ani nzima na hadithi 40 maarufu kama Hadith an-Nawawiya, hifdhi ya Qur'ani nzima na hadithi 490 kutoka kitabu cha Riyadhu Swalihin, hifdhi ya Qur'ani nzima sambamba na kufafanua maana na hatimaye hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na Mandhumatu al-Jazariya.
Jumuiya ya Qur'ani ya Maadh imesema kuwa waamuzi wa mashindano hayo ni wataalamu mashuhri wa Qur'ani kutoka nchini Yemen.
Mashindano hayo yamepangwa kuendelea hadi hapo kesho Jumatano. Sherehe za kihitimisha mashindano hayo zimepangwa kufanyika siku ya Alkhamisi Juma lijalo yaani tarehe 8 Shaaban. Jumuiya ya Maadh imewataka Wayemen kuchangia na kusaidia kifedha shughuli za Qur'ani kama hizo ili kulea kizazi kinachozingatia Qur'ani nchini humo. 1032966