Okiba Janan ameiambia IQNA kwamba japokuwa tabaka la vijana katika nchi mbalimbali duniani linafuatilia habari za kisiasa na kiutamaduni na linaelewa vyema matukio yanayojiri katika nchi za Libya, Tunisia, Misri, Yemen na Bahrain lakini halina maaarifa ya kutosha kuhusu mwamko wa Kiislamu na linachambua matukio hayo kwa mtazamo wa kisiasa.
Amesema kwa msingi huo mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ndio chanzo cha mwamko wa Kiislamu katika dunia ya sasa yanawaelimisha mengi washiriki kuhusu wimbi la mwamko wa Kiislamu, misingi ya mapinduzi ya wananchi dhidi ya tawala za Kiimla na kuwatayarisha maqarii kwa ajili ya kubainisha mafunzo ya Uislamu katika nchi nyingine.
Katika upande mwingine Qarii huyo wa Ufaransa amesema wasomi wa Qur'ani wanaweza kufikisha vyema zaidi ujumbe wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu kwa watu wa jamii kuliko watu wengine. Amesisitiza kuwa ujumbe wa Qur'ani unaweza kufikishwa kwa watu wa jamii kwa kutumia mbinu mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na hotuba za maulamaa. Amesema ni maqarii wa Qur'ani peke yao ndio wanaoweza kufikisha ujumbe wa Qur'ani kwa watu kwa njia ya moja kwa moja na kwa msingi huo kutayarisha maqarii na wasomaji wa Qur'ani kuna umuhimu mkubwa zaidi katika suala zima la kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu.
Amesifu kiwango cha mashindano ya Qur'ani ya Tehran na kusema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mstari wa mbele katika shughuli za kiqur'ani kati ya nchi zote za Kiislamu. 1033074