IQNA

Qur'ani yatarjumiwa kwa lugha ya ishara Marekani

12:24 - December 06, 2012
Habari ID: 2459080
Mradi wa kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara ya Kimarekani umeanza kutekelezwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu wenye Ulemavu wa Kusikia nchini marekani (GDM).
Tovuti ya Examiner imeripoti kuwa mradi huo unajumuisha matayarisho ya video ya wasomaji Qur'ani kwa lugha ya ishara ya inayotumiwa Marekani huku tarjumi ya aya za kitabu hicho kwa lugha ya Kiingereza ikionekana chini ya mkanda huo wa video.
Baada ya kukamilika mradi huo, tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara ya Marekani (ASL) itawekwa kwenye mtandao wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu Wenye Ulemavu wa Kusikia nchini Marekani (GDM).
Tarjumi hiyo ya Qur'ani itatolewa bure kwa walemavu wa kusikia.
Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu Wenye Ulemavu wa Kusikia nchini Marekani (GDM) ndio taasisi pekee inayojishughulisha na kazi za kutayarisha masomo na zana za kusomea kwa ajili ya viziwi Waislamu.
Ni vyema pia kuashiria hapa kuwa lugha ya ishara ya Kimarekani ni tofauti kabisa na lugha ya Kiingereza ina nahau yake ya kipekee. 1147584

captcha