Maeneo mbalimbali ya Ethiopia yamekumbwa na maandamano ya mara kwa mara tangu baada ya kuanza wimbi la mwamko wa Kiislamu katika nchi za kaskazini mwa Afrika.
Ili kuzuia wimbi hilo, serikali ya Ethiopia imeweka vizuizi vingi ikiwa ni pamoja na mipaka ya kufanyika mahfali za kidini na vikao vya kiraa ya Qur'ani nchini humo.
Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Adis Ababa pia kimelazimika kusimaisha darsa za tafsiri ya Qur'ani na sayansi ya kitabu hicho kutokana na mashinikizo ya serikali ya Ethiopia. 1162175