IQNA

Iran mwenyeji wa Mashindano ya Qur’ani ya Majeshi ya Nchi za Kiislamu

14:34 - January 15, 2013
Habari ID: 2480765
Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Majeshi ya Nchi za Kiislamu yatafanyika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia Januari 21-24.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu na Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Jamhuri ya Kiislamu Brigedia Jenerali Hussein Salamu, maqari na mahufadh 80 kutoka nchi 21 za Kiislamu watashiriki katika mashindano.
Brigedia Jenerali Salamu ameashiria sisitizo la Qur’ani Tukufu kuhusu umoja wa Waislamu na kusema mashindano hayo ya Qur’ani yanaweza kutoa mchango mkubwa katika kuimarisha Umoja wa Kiislamu mbali na kuwawezesha washiriki kufahamu malengo matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kamanda huyo wa ngazi za juu amesema mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hayati Imam Khomeini SA na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khamenei wote wamesisitiza kuhusu umuhimu wa umoja wa Kiislamu. Mashindano hayo yatajumuisha qiraa ya Qur’ani Tukufu pamoja na kuhifadhi Juzuu 5, Juzuu 15 na Qur’ani Kamili. Mashindano hayo ya Qur’ani yatafanyika mjini Tehran na waliothibitisha kushiriki ni wanajeshi kutoka Pakistan, Senegal, Brunei, Ivory Coast, Iraq, Syria, Oman, Sudan, Indonesia, Palestina, Algeria, Mali, Malaysia, Jordan, Afghanistan na Bangladesh.
1171177
captcha