IQNA

Kituo cha Qur'ani Tukufu kuanzishwa Zamfara, Nigeria

9:40 - February 05, 2013
Habari ID: 2491615
Gavana wa jimbo la Zamfara nchini Nigeria ametangaza azma ya jimbo hilo ya kuanzisha kituo cha usomaji Qur'ani.
Gazeti la Daily Time limemnukuu Abdul Aziz Yari akisema katika hafla ya kuhitimisha mashindano ya tajwidi ya Qur'ani Tukufu kuwa jimbo hilo litaanzisha kituo cha Qur'ani Tukufu. Amesema kituo hicho kitasaidia juhudi za ueneza uelewa wa Qur'ani na kusahilisha utekelezaji wa asheria za Kiislamu katika jimbo hilo.
Wakati huo huo kesho kutafunguliwa studio ya kukusanya visomo na kiraa za Qur'ani katika jimbo la Kano. Studio hiyo itafunguliwa kwa jitihada za kundi la sturio za Qur'ani la Goni Abacha.
Mkuu wa Baraza la Wadhamini wa taasisi hiyo Muhammad Abacha amesema mradi wa ufunguzi wa studia hiyo ya Qur'ani Tukufu umegharimu naira milioni 250.
Studio hiyo itakuwa na kazi ya kueneza kiraa ya Qur'ani Tukufu, kuhifadhisha kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kueneza moyo wa kuishi pamoja kwa amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali nchini Nigeria. 1182831


captcha