Televisheni ya kimataifa ya al Alam imeripoti kuwa, hatua hiyo ya Mawahabi wa Saudia inaweka wazi mitazamo yao ya kutaka kubadili utambulisho wa mji wa kihistoria na wa Kiislamu wa Madina ambao kwa karne nyingi sasa umekuwa nembo kubwa na mahala patakatifu kwa Waislamu wote duniani.
Wafuatiliaji wametahadharisha kwamba hatua hiyo ya Mawahabi inaweza kuwa utangulizi wa kubomolewa msikiti huo kwani katika miaka ya huko nyuma pia Mawahabi wenye misimamo ya kufurutu ada waliokuwa wakiungwa mkono na utawala wa Aal Saud waliharibu na kuvunja turathi nyingi za kale za Kiislamu.
Mipango ya Mawahabi ya kuharibu turathi za kihistoria za Kiislamu katika mji wa Madina na kufuta picha ya kuba ya Msikiti wa Mtume (saw) katika nembo ya mji huo mtakatifu imekabiliwa na upinzani mkubwa wa wanaharakati wa Kiislamu.
Mawahabi wanaodai kuwa kuzuru kaburi la Mtume Muhammad (saw) na mawalii wa Mwenyezi Mungu ni bidaa na uzushi, wanawazuia Waislamu kutembelea maeneo hayo na wamekuwa wakiyaharibu taratibu kwa kisingizio cha kupanua msikiti wa Mtume. Hadi sasa misikiti kadhaa ya kihistoria ya Madina imeharibiwa kwa kisingizio hicho. 1184651