Mashindano hayo yanasimamiwa na Waziri wa Ulinzi wa Saudia Salman bin Abdulaziz Aal Saud na yataendelea kwa kipindi cha siku 6.
Wamajeshi 91 kutoka nchi 26 za Kiarabu, Kiislamu na zisizo za Kiislamu wanashiriki katika mashindano hayo.
Miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ni kuwahamasisha wanajeshi kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kutadabari maana ya aya za kitabu hicho na kuamiliana kwa mujibu wa mafundisho yake.
Pambizoni mwa mashindano hayo kutakuwepo semina za kidini, warsha za mafunzo, maonyesho ya teknolojia za Qur'ani na kadhalika. Washiriki katika mashindano hayo pia watatembelea kiwanda cha kuchapisha Qur'ani cha Mfalme Fahad, karakana ya kutengeneza pazia la al Kaaba na kiwanda kinachotayarisha maji ya Zamzam katika miji mitukufu ya Makka na Madina. 1193335