IQNA

Warsha ya kuboresha mafundisho ya Qur'ani kufanyika Marekani

22:21 - March 02, 2013
Habari ID: 2504851
Warsha ya kuboresha mafundisho ya Qur'ani imepangwa kufanyika tarehe 28 Machi katika mji wa Rosemont katika jimbo la Illinois nchini Marekani.
Warsha hiyo itasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya America Kaskazini (ISNA).
Warsha hiyo na nyingine tatu zitafanyika kabla ya kuanza kongamano la nne la kila mwaka la Mafunzo ya Kiislamu la Jumuiya ya Kiislamu ya America Kaskazini.
Warsha hiyo itachunguza masuala kama ratiba za mafunzo ya Qur'ani, mipango ya kupanga utaratibu wa kutoa mafunzo ya Qur'ani, mbinu mbalimbali za kufunza Qur'ani na kadhalika.
Kongamano la mafunzo ya Kiislamu la Jumuiya ya Kiislamu ya America Kaskazini (ISNA) hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuboresha mafunzo ya Kiislamu nchini Marekani. 1197205

captcha