Rais Rouhani ameyasema hayo katika ujumbe alioutuma kwa watu wote duniani wakiwemo viongozi wa nchi mbalimbali za Wakristo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis I kwa mnasaba wa siku ya kukumbuka kuzaliwa Nabi Issa AS na kuwadia mwaka mpya wa 2015. Katika ujumbe wake huo Rais Rouhani ametoa wito kwa watu wote duniani kushirikiana kwa lengo la kuelekea katika dunia bora. Rais wa Iran amekumbusha kuwa Nabi Issa AS alikuwa anafuatilia dunia iliyojaa amani. Huku akiashiria pendekezo lililowasilishwa na Iran na kuidhinishwa kwa wingi wa kura katika Umoja wa Mataifa kuhusu dunia isiyo na misimami mikali na machafuko, Rais Rouhani amesema Iran iko tayari kuchukua hatua za kivitendo kwa ajili ya kustawisha amani na maisha ya maelewano duniani.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani naye pia ametuma ujumbe kwa maspika wa nchi za Wakristo kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Nabi Issa AS na kuanza mwaka mpya. Katika ujumbe wake Dakta Larijani amesema hivi sasa mataifa mengi yanasumbuliwa na machafuko na misimamo mikali. Amesema, leo hii dunia inahitaji utulivu sambamba na uadilifu, amani, udugu, kumwamini Mwenyezi Mngu na kupambana na dhulma.../mh