kuhisi wanavyohisi wanaovaa hijabu sambamba na kupinga ubaguzi kwa wale wanaochagua hijabu kwa msingi wa dini na mtindo wa maisha.
Katika taarifa kupitia ukurasa wao wa Facebook, waandalizi wa ‘Siku ya Hijabu Duniani’ wamesema: “Lengo letu ni kuwa na washiriki Milioni 10 kote duniani siku ya Februari 1, Insha’Allah! Maadhimisho haya yameandaliwa kutokana na mafanikio ya miaka miwili iliyopita na yanafanyika kwa nara za ‘ufahamu bora’ na ‘amani duniani’ ili kuwepo maelewano ya kidini kupitia Hijabu.”
Katika siku hiyo ya hijabu duniani wanawake wasio kuwa Waislamu na wanawake Waislamu ambao kawaida hawavai Hijabu wameahidi kuvaa Hijabu ili kupata uzoefu wa wale wanaovaa hijabu.
Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Siku ya Hijabu Duniani’ (World Hijab Day-WHD-), siku hii ilianzishwa na mkaazi wa New York Marekani, Bi. Nazma Khan kwa lengo la kuwahimiza watu kuwasilisha fikra za namna wafuasi wa dini mbali mbali wanavyoweza kuishi pamoja kwa maelewano na huo ndio msingi wa kuwaalika wasiokuwa Waislamu kuvaa Hijabu walau kwa siku moja. Siku ya Hijabu Duniani inatazaiwa kuadhimishwa katika mabara yote duniani.../mh