IQNA

Mahafidhi 60 wa Qur'ani waenziwa kusini mwa Misri

12:29 - February 03, 2015
Habari ID: 2802772
Mahafidhi 60 wa Qur'ani Tukufu, wanawake kwa wanaume, wameenziwa katika mkoa wa Qena ulioko kusini mwa Misri.

Mahafidhi 60 wa Qur'ani Tukufu, wanawake kwa wanaume, wameenziwa katika mkoa wa Qena ulioko kusini mwa Misri.
Sherehe ya kuwaenzi maqari hao wa Qur'ani ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu wa Misri Imad Shakir na viongozi wengine wa mkoa wa Qena.
Mahafidhi hao 60 wa Qur'ani waliongoza katika mashindano yaliyoshirikisha maqari 1100 katika kitengo cha hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzu 15, hifdhi ya robo ya Qur'ani na hifdhi ya juzu kadhaa za Qur'ani.
Mwishoni mwa sherehe hiyo washindi walitunukiwa zawadi ya lira elfu saba kutoka Wizara ya Elimu ya Misri na lira nyingine 2600 kutoka Jumuiya ya Vijana Waislamu ya nchi hiyo. AIR

2797187

Kishikizo: Qur'ani, Qena, juzuu
captcha