IQNA

Utawala wa Kizayuni umeua watoto 980 Ukanda wa Ghaza

0:18 - June 07, 2015
Habari ID: 3311464
Jeshi la Utawala haramu wa Israel limewaua watoto wapatao 980 katika hujuma zake za hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kawaida hukiuka sheria zote za kimataifa kuhusu kulinda haki za watoto katika vita vyake dhidi ya Ghaza. Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Kimatiafa ya Kuwatetea Watoto Wapalestina, kwa mnasaba wa Siku ya Watoto Wasio na Hatia ambayo huadhimishwa Junia 4, imesema kuwa mwaka 2014 ndio uliokuwa mbaya na mgumu zaidi kwa watoto wa Ghaza kwani zaidi ya watoto 530 waliuawa shahidi katika hujuma za jeshi katili la Israel. Aidha taasisi hiyo imesema katika mwaka huo, kwa wastani watoto 196 Wapalestina walikuwa wakikamatwa kila mwezi na vikosi vya Israel. Kwa ujumla zaidi ya Wapalestina 2,100, wengi wao wakiwa raia, waliuawa shahidi katika hujuma ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza mwaka 2014.  Aidha mwaka 2012 na mwishoni mwa 2008 hadi mwanzoni mwa 2009 utawala haramu wa Israel ulitekeleza hujuma za kikatili dhidi ya Wapalestina walio chini ya mzingiro katika Ukanda wa Ghaza.

Wakati huo huo taasisi za Umoja wa Mataifa zimeafikiana na taasisi za Palestina kuwa idadi ya kushtusha ya watoto waliuawa katika hujuma ya Israel huko Ghaza mwaka jana. Katika ripoti ya siri yenye kurasa 22 iliyovujishwa kwa vyombo vya habari, Jeshi la Israel limetajwa kuwa ni mtenda jinai dhidi ya watoto. Ripoti hiyo pia imetaja namna jeshi la Israel lilivyodondosha mabomu katika shule saba za Umoja wa Mataifa katika vita vya mwaka jana Ghaza ambapo watu 44 waliokuwa wamepata hifadhi hapo waliuawa shahidi. Imedokezwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko chini ya mashinikizo ya Marekani kutoiweka Israel katika orodha ya nchi zinazokiuka haki za watoto kama ilivypendekezwa katika ripoti hiyo.../mh

3311206

captcha