Akizungumza na IQNA baada ya kuibuka mshindi katika kitengo cha qiraa, Mohsen Haji-Hassani Kargar amesema lengo lake katika mashindano si kupata nafasi ya kwanza bali ni kusonga mbele katika njia ya Qur'ani Tukufu.
Amesema ameridhika ni kisomo chake na ameelezea matumaini yake kuwa washiriki wa mashindano hayo wataendeleza utamaduni wa Qur'ani katika nchi zao. Haji Hassani Kargar ameyataja mashindano ya Qur'ani kuwa ni fursa kwa Waislamu kuelekea katika utekelezaji mafundisho ya Qur'ani na pia kuimarisha umoja wa Waislamu duniani../mh