IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Umoja , tiba ya matatizo ya Waislamu

23:58 - July 18, 2015
Habari ID: 3329122
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, umoja na mshikamano ni tiba ya matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mbele ya hadhara ya viongozi wa Iran, mabalozi wa nchi za Kiislamu waliopo hapa mjini Tehran na matabaka mbalimbali ya wananchi na kubainisha kwamba, vita vya hivi sasa vya kimadhehebu na kikabila katika Mashariki ya Kati ambavyo ni vya kupangwa na kutwishwa Waislamu, lengo lake ni kuzipotosha fikra za mataifa ya Kiislamu na kuyafanya yasiuzingatie utawala wa Kizayuni wa Israel. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kutoa mkono wa kheri, baraka na fanaka kwa mnasaba wa Sikukuu ya Eid ul Fitr ameashiria mazingira ya kusikitisha ya ulimwengu wa Kiislamu na suala la kutokuwepo umoja na mshikamano na kuongeza kuwa, mifarakano na hitilafu zilizoko hivi sasa katika Mashariki ya Kati sio za kawaida, bali ni za kutwishwa. Ayatullah Khamenei amewataka maulamaa, wanafikra, viongozi wa serikali, wanasiasa na watu wenye vipawa katika ulimwengu wa Kiislamu kuwafahamu na kuwazingatia watu wanaousaliti umma wa Kiislamu ambao wanafanya njama za kuleta mifarakano na mizozo hiyo. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siasa za madola ya kiistikbari katika eneo la Mashariki ya Kati ni za kiusaliti na khiyana hivyo watu wote wanapaswa kulizingatia vizuri jambo hilo. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, siasa na sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashariki ya Kati ziko dhidi ya siasa za kiistikabari. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria suala la Iraq na kusema kuwa, siasa za uistikabri nchini Iraq ni kuiondoa madarakani serikali halali iliyochaguliwa na wananchi, kuzusha mifarakano baina ya Mashia na Masuni na hatimaye kuigawa nchi hiyo ya Kiarabu; katika hali ambayo siasa za Iran kuhusiana na Iraq ni kuiunga mkono na kuiimarisha serikali iliyopatikana kwa kura za wananchi, kuiunga mkono serikali hiyo katika jitihada zake za kupambana na vibaraka wanaofanya njama za kueneza vita vya ndani na wanaozusha mizozo kama ambavyo inaunga mkono pia kulindwa ardhi yote na kutogawanywa nchi hiyo.../mh

3329090

captcha