Ameashiria kukombolewa ardhi za Lebanon zilizokuwa zikikaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni na ushindi wa Wapalestina wa Ghaza katika vita na utawala wa Kizayuni kuwa mafanikio mengine ya harakati za mapambano.
Kiongozi wa Hizbullah ameongeza kuwa hakuna suala muhimu ulimwenguni kama kadhia ya Palestina. Sayyid Hassan Nasrullah amesema hay oleo Jumanne mjini Beirut Lebanon katika kongamano la "Umoja kwa Ajili ya Palestina" na kubainisha kwamba, hivi sasa kuna mapigano na hitilafu nyingi katika maeneo mbalimbali duniani na katika hayo haki na batili vimechanganyika, lakini jambo pekee ambalo linaitenganisha kikamilifu haki na batili ni kadhia ya Palestina. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, moja ya vigezo vya kuzitathmini serikali, vyama, makundi, shakhsia na nchi mbalimbali ni kuangalia msimamo wao kuhusiana na kadhia ya Palestina ukoje. Kiongozi huyo wa Hizbullah amesema bayana kwamba, watu wote wana jukumu la kukabiliana na mipango ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba, lengo la kukabiliana na Israel ni kuisambaratisha mipango ya maghasibu hao katika Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu wa Hizbullah amezungumzia matukio ya Yemen na Iraq na kuzitaja kuwa kambi mbili muhimu za mhimili wa muqawama. Nasrullah amesema pia kwamba, matukio yaliyojiri Syria na yanayoendelea kutokea nchini humo ni madhara kwa mhimili wa muqawama kwani Syria ina nafasi muhimu mno katika mhimili wa muqawama na mapambano.../mh