IQNA

Magaidi wa Boko Haram hawawezi hata kusoma Surat al-Fatiha

18:13 - August 31, 2015
Habari ID: 3355686
Magaidi wa Boko Haram hawawezi hata kusoma Qur'ani Tukufu wala kutekeleza maundisho ya dini ambayo wanadai kupigania wanapotekeleza jinai zao, amesema afisa mwandamizi wa jeshi la Nigeria.

"Aghalabu ya magaidi wa Boko Haram waliokamatwa na Jeshi la Nigeria hawawezi hata kusoma Qur'ani Tukufu, wengine wao hata hawawezi kusoma sura ya kwanza ya Qur'ani Tukufu, Surat al-Fatiha, katika hali ambayo wanadai kuwa wanataka kuanzisha "dola la Kiislamu," amesema kaimu mkurungezi wa habari katika Jeshi la Nigeria, Kanali Sani Kukasheta Usman.
Afisa huyo mwandamizi wa Jeshi la Nigeria amesema vitendo vya Boko Haram ni vya kuaibisha na kushangaza. Aidha amefichua kuwa, "wakati Jeshi la Nigeria lilipoteka ngome za Boko Haram, hakuna hata nakla moja ya Qur'ani iliyopatikana wala vitabu vingine vya Kiislamu."
"Tulipata silaha, bidhaa za kichawi, kondomu,  kila aina ya mihadarati na hata dawa za kuimarisha nguvu za kiume katika msitu wa Sambisa jimboni Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria," amesema Usman.
Katika ujumbe aliotuma kupitia mtandao wake wa kijamii, Usman amesema kundi la Boko Haram linauharibia Uislamu jina.
Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.
Zaidi ya watu 15 elfu wameuawa tangu Boko Haram waanzishe uasi kaskazini mwa Nigeria.
Hivi karibuni Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa mara nyingine tena ameituhumu Marekani kuwa inawaunga mkono magaidi wa kundi la Boko Haram. Akizungumza Agosti 10 kwenye sherehe za kufuzu wanajeshi wa cheo cha Cadet, Rais Buhari alisema Washington imekuwa ikiwaunga mkono matakfiri wa Boko Haram na kuitaka Wizara ya Ulinzi kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha jeshi linajitosheleza katika masuala ya silaha. Rais wa Nigeria amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kukataa kuiuzia nchi yake silaha inawapa nguvu magaidi wa Boko Haram na hapana shaka kwamba hilo ndilo lengo kuu la serikali ya Washington.../mh

3354429

captcha