Jeshi la Iraq limesema kuwa, kikosi chake cha anga kimeshambulia msafara wa al-Baghdadi ambaye pia anajulikana kwa jina la Ibrahim al-Samarrai, katika mkoa wa Anbar ulioko magharibi mwa nchi hiyo.
Hata hivyo taarifa ya jeshi hilo imesema, hatima ya kiongozi huyo wa Daesh haijulikani na kwamba kwa sasa anauguza majeraha katika sehemu isiyojulikana.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, mapema leo kundi hilo la kitakfiri limewaangamiza wanachama wao 60 baada ya kuwashuku kuwa wanataka kuliasi kundi hilo.
Al-Baghdadi ambaye alijitangaza kuwa mkuu wa kundi la hilo la Daesh mwaka jana, alijeruhiwa katika shambulizi la anga la Marekani mwezi Machi mwaka huu.