IQNA

Majlis za Muharram katika Msikiti wa Masunni, Khatibu Mshia

13:31 - October 21, 2015
Habari ID: 3391260
Katika jitihada za kuleta umoja baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, kumefanyika Majlisi za maombolezo Mwezi wa Muharram katika msikiti wa Masunni ambapo khatibu alikuwa ni mwanazuoni wa Kishia katika Kituo cha Kiislamu cha Dearborn, Michigan nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, majlis hiyo ilifanyika Ijumaa Oktoba 17 ambapo akizungumza katika kikao hicho, mkuu wa kituo hicho cha Kiislamu Sheikh Mohammad Mardini amesisitiza kuhusu umuhimu wa Waislamu kudumisha umoja na kujiepusha na mifarakano.
Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani katika kipindi hiki hushiriki katika  vikao au majlisi za mwezi wa Muharram ambao kilele chake ni siku ya 10 ijulikanayo kama Ashura wakati Waislamu hukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Mtume Muhammad , SAW, Imam Hussein AS huko Karbala. Aghalabu ya majlisi hizo za Muharam huandaliwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Majlisi hiyo ya Muharram mjini Dearborn Marekani ilihudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni.
Akihutubu katika majlis hiyo, mwanazuoni wa Kishia Sheikh Mohammad Dbout amesema kufanyika Majlisi ya Imam Hussein AS katika msikiti wa Kisunni ni ujumbe kuwa Waislamu wameungana na kwamba tukio la Ashura si la kimadhehebu. "Sisi sote tuko katika dini moja ambayo ujumbe wake ni amani na kustahamiliana," amesema.
Kwa upande wake Sheikh Mardini amesema Imam Hussein AS anaenziwa na kuheshimiwa na Waislamu wote na kwamba mapinduzi yake si ya madhehebu moja tu. Ameongeza kuwa mapinduzi ya Imam Hussein AS yalikuwa ni dhidi ya udhalimu. "Katika kipindi hiki ambacho Waislamu wanakabiliana na kila aina ya dhulma na ubaguzi, kuna haja ya kuwa na umoja na mashikamano hasa katika siku ya Ashura," amesema Sheikh Mardini.../mh

3391114

captcha