Ameyasema hayo mjini Tunis alipokutana na Balozi wa Iran mjini humo Moustafa Borujerdi aliyemkabidhi mwaliko wa kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu.
Waziri wa Masuala ya Dini Tunisia amesema Iran ina nafasi ya juu katika ulimwengu wa Kiislamu. Ameongeza kuwa kuna ulazima wa kukabiliana na misimamo mikali katika ulimwengu wa Kiislamu.
Katika kikao hicho, balozi wa Iran mjini Tunis amesema maulamaa wa Tunisia wamekuwa na nafasi muhimu katika kuleta ukuruba na umoja wa Kiislamu. Aidha amesema 'Wiki ya Umoja wa Kiislamu' ni chanzo cha mshikamano wa umma wa Kiislamu. Ameendelea kusema kuwa mafundisho ya Ahul Bayt AS yamejengeka katika msingi wa umoja na mshikamano wa umma wa Kiislamu na ni kwa sababu hii ndio nchini Iran kuna umoja na udugu baina ya Mashia na Masunni. Balozi huyo pia ameashiria kadhia ya kuuawa maelfu ya Waislamu wakati wa Ibada ya Hija iliyopita huko Mina na kusema kufuatia tukio hilo la kusikitisha, kuna haja ya maulamaa wa Kiislamu kutafakari kuhusu njia bora ya utekelezaji ibada ya Hija.