IQNA

Polisi waua Mashia zaidi Nigeria, Boko Haram nao waua wanavijiji

14:30 - December 16, 2015
Habari ID: 3463969
Polisi nchini Nigeria wameendeleza ukatili wa jeshi la nchi hiyo kwa kuwaua Waislamu wanne wa madhehebu ya Shia huku magaidi wa Boko Haram wakiachwa huru kuendeleza mauaji yao.

Imearifiwa kuwa  Waislamu wanne wa madhehebu ya Shia wameuawa katika mji wa Kaduna mashariki mwa Nigeria katika maandamano ya kulaani mauaji ya mamia ya Mashia siku za Jumamosi na Jumapili. Waandamanaji hao pia wametaka kuachiliwa huru mara moja kiongozi wa Mashia Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake ambao wanashikiliwa katika korokoro za jeshi la nchi hiyo.
Imearifiwa kuwa siku za Jumamosi na Jumapili idadi ya Waislamu waliouawa katika shambulio dhidi ya Nyumba ya Kiognozi wa Mashia Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky na kituo cha Mashia nchini Nigeria inafikia watu 500. Wengine wanaamini kwamba, idadi hiyo yumkini ikaongezeka na kufikia hata watu elfu moja. Aidha Sheikh Zakzaky ambaye amejeruhiwa anashikiliwa na jeshi la nchi hiyo.
Kwingineko Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria wamewaua watu 30 katika hujuma dhidi ya vijiji vitatu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Hujuma hizo zimejiri Jumanne katika vijiji vya Warwara, Mangari na Bura-Shika jimboni Borno ambapo watu wengine 20 pia wamejeruhiwa. Magaidi hao pia wameteketeza vijiji hivyo baada ya kuwaua wanavijiji. Alhamisi iliyopita magaidi wakufurishaji wa Boko Haram walishambulia kijiji cha Kamuya katika jimbo hilo hilo na kuua watu 14. Hayo yanajiri katika hali ambayo badala ya jeshi kukabiliana na magaidi hao wa Boko Haram linajishughulisha kuwaua Waislamu wasio na hatia wa madhehebu ya Shia.
Magaidi wa Boko Haram wamewaua watu zaidi ya 20,000 tokea waanzishe uasi wao mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria.

3463811

captcha