IQNA

Waislamu Nigeria walaani Rais Buhari kwa kupendekeza marufuku ya Hijabu

13:17 - January 03, 2016
Habari ID: 3470006
Jumuiya ya Haki za Waislamu Nigeria imetoa taarifa na kulaani vikali mpango wa Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo kutaka kupiga marufuku vazi la Hijabu.

Kwa mujibu wa mwandisho wa IQNA, Jumuiya ya Haki za Binadamu Nigeria mbali na kulaani pendekezo hilo la Rais Buhari imesema sera kama hiyo ni njia ya kukwepa utatuzi wa matatizo ya kimsingi ya nchi hiyo.  Nayo Jumuiya ya Mawakili Nigeria (NBA) imesema kupigwa marufuku vazi la kujisitiri wanawake Waislamu yaani Hijani ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo. Okey Wali mkuu wa Jumuiya hiyo amesema serikali inapaswa kutafuta suluhisho la kudumu na la amani kuhusu changamoto za usalama nchini humo .
Kauli hizo zimetolewa baada ya serikali kusema kuwa baadhi ya wanaotekeleza hujuma za kigaidi ni wanawake wanaovaa Hijabu.
Wali amesema kupiga marufuku Hijabu kwa msingi huo si hatua chanya wala suluhisho la kudumu la ukosefu wa usalama. Amesema kwa mujibu wa katiba ya Nigeria, kila mtu ana haki ya kuvaa mavazi kwa mujibu wa dini yake na hivyo hakuna uwezekano wa kuwazuia wanawake Waislamu kuvaa Hijabu.
Hiyo juzi baada ya kupuuza mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria, Rais Muhammadu Buhari ametoa matamshi yaliyowashangaza wengi na kusema iwapo italazimu atapiga marufuku vazi la mwanamke wa Kiislamu la hijabu.
Rais Buhari aliongeza kuwa, serikali yake haina njia nyingine ghairi ya kuchagua moja kati ya mambo mawili ama vazi la hijabu au usalama na kwamba yeye atalipiga marufuku vazi hilo la staha la mwanamke wa Kiislamu nchini Nigeria.
Buhari amesema wanawake hawapasi kuvaa hijabu kwa sababu vazi hilo linatumiwa kulipua mabomu na kwamba wanawake hao ni magaidi.
Baada ya mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria wiki kadhaa zilizopita katika mji wa Zaria wanawake wengine wametiwa nguvuni na kuvuliwa vazi lao la hijabu katika korokoro za nchi hiyo. Hii ni licha ya kwamba inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya Wanigeria ni Waislamu. Hatua za hivi karibuni za serikali ya Nigeria zimefichua mkono wa Wazayuni na Marekani dhidi ya Waislamu nchini Nigeria.
Tarehe 13 Disemba jeshi la Nigeria lilishambulia vituo vya Harakati ya Kiislamu Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuua mamia ya Waislamu na kisha kumtia mbaroni kiongozi huyo.

3471377

captcha