IQNA

Waislamu Nigeria waionya serikali isijaribu kupiga marufuku Hijabu

9:14 - January 12, 2016
Habari ID: 3470032
Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu Nigeria wameionya serikali hiyokuhusu hatua yoyote ya kupiga marufuku vazi la Hijabu ya wanawake Waislamu nchini humo.

Mkuu wa Bodi ya Jumuiya ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu Nigeria MSSN Abdulqadir Orire ametoa tahadhari hiyo wakati wa mkutano wa bodi hiyo siku ya Jumapili katika eneo la Ilorin.

Orire ambaye amekuwa Kadhi Mkuu wa kwanza wa Mahakama ya Rufaa ya Sheria za Kiislamu katika jimbo la Kwara amesema hatakubali marufuku ya chochote ambayo ni sehemu ya mafundisho ya Kiislamu yaliyoteremshwa na Allah SWT.

Amelaani wito uliotolewa na baadhi wakitaka kupigwa marufuku hijabu ambayo ni sehemu ya mavazi ya wanawake Waislamu.

Hivi karibuni baada ya kupuuza mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria, Rais Muhammadu Buhari amesema iwapo italazimu atapiga marufuku vazi la mwanamke wa Kiislamu la hijabu.

Rais Muhammad Buhari aliyasema hayo jana na kuongeza kuwa, serikali yake haina njia nyingine ghairi ya kuchagua moja kati ya mambo mawili ama vazi la hijabu au usalama na kwamba yeye atalipiga marufuku vazi hilo la staha la mwanamke wa Kiislamu nchini Nigeria.

Buhari amesema wanawake hawapasi kuvaa hijabu kwa sababu vazi hilo linatumiwa kulipua mabomu na kwamba wanawake hao ni magaidi.

http://iqna.ir/fa/news/3466542

captcha