IQNA

Malalamiko Mauritania baada ya kuondolewa somo la "Malezi ya Kiislamu"

7:08 - January 25, 2016
Habari ID: 3470084
Wizara ya Elimu Mauritania imekosolewa vikali kufuatia uamuzi wake wa kuondoa somo la "Malezi ya Kiislamu" katika mitihani ya shule za sekondari nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wazazi, wananchi na wanafunzi Mauritani wamelalamikia uamuzi huo wa kufutwa somo hilo muhimu katika kulea kizazi cha Waislamu bora.

Somo la "Malezi ya Kiislamu" mwaka huu limefutwa katika mitihani ya shule za sekondari Mauritania ambapo huko nyuma wanafunzi nchini humo, walikuwa wametaka alama za somo la malezi ya Kiislamu lijumuishwe katika jumla la alama za mwisho wa temu mbali na kutaka pia masaa ya kufunza masomo hayo kuongozwa. Ould Mohammad, mwanafunzi wa Kimauritania amelalamika kuwa wizara ya elimu ya Mauritania imekata masomo ya malezi ya Kiislamu katika shule za sekondari katika hali ambayo mwaka jana wizara hiyo ilikuwa imepanga kuongeza masaa ya somo hilo.

Ikumbukwe kuwa Desemba mwaka jana, kulifanyika maandamano maeneo kadhaa ya Mauritania kulaani hatua ya serikali kufunga vituo kadhaa vya Qur’ani na chekechea.

Viongozi wa kidini na wahubiri nchini humo nao pia wameonya kuhusu kuvurugwa masomo ya kidini na Qur’ani nchini humo.

Mauritania ni nchi ya eneo la Maghreb huko magharibi mwa Afrika Kaskazini na inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4 ambao karibu wote ni Waislamu.

3469785

captcha