IQNA

Kikao kuhusu 'Harakati za Qur'ani Afrika' mjini Qum

19:57 - February 01, 2016
Habari ID: 3470106
Kongamano la kitaalamu kuhusu 'Harakati za Qur'ani Barani Afrika' kimefanyika katika mji wa Qum kusini mwa Tehran, Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limefanyika hivi karibuni kwa himaya ya tawi la Darul Qur'an katika Taasisi ya Haram Takatifu ya Imam Hussein AS mjini Qum ambapo walishiriki wahadhiri wa vyuo vikuu, maulamaa na wanafunzo katika vyuo vya kidini.

Kogamano hilo pia limeandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Wanafunzi Waafrika ambapo Ustadh Maaruf Abdul Majid, mtaalamu wa Qur'ani kutoka Misri ameongoza kikao hicho.

Hajj Mussa Fal, mtaalamu wa Qur'ani ambaye pia ni mwambata wa kiuchumi katika ubalozi wa Senegal mjini Tehran ameshiriki katika kikao hicho na kuwasilisha makala ya kitaalamu yenye anuani ya "Ustawi wa Mafundisho ya Qur'ani Afrika Magharibi; Senegal kama Mfano."

Halikadhalika ameangazia nukta kadhaa kama vile namna Uislamu ulivyoingia barani Afrika, kuenea madrassah za Qur'ani Senegal na mbinu za kufundisha Qur'ani katika madrassah za kale nchini humo.

Kwa upande wake, Ja'afar Turai, mtaalamu wa Qur'ani kutoka nchini Mali amewasilisha makala kuhusu "Nafasi ya Qur'ani Barani Afrika". Wengine waliowasilisha makala za utafiti kuhusu nafasi ya Qur'ani barani Afrika katika kikao hicho ni pamoja na Sheikh Ibrahim Ankam wa Senegal, Sheikh Ismail Balam wa Burkina Faso, Sheikh Ali Ahmad Ba wa Mauritania , Sayyid Hamid Jallo na Mohammad Ibrahim wa Nigeria.

3471335

captcha