IQNA

Mashindano ya Qur'ani Afrika Magharibi yafanyika Senegal

10:20 - June 23, 2016
Habari ID: 3470411
Awamu ya 24 ya Mashindano ya Qur'ani ya nchi za Afrika Magharibi yamefanyika nchini Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za kufunga mashindano hayo zimefanyika kwa kuhudhuriwa na Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Dakar Bw. Hassan Esmati. Mashindano hayo ya kila mwaka huandaliwa na Jumuiya ya Vijana Waislamu Senegal na kuhudhuriwa na quraa na hufadh wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi kama vile Senegal, Mali, Mauritania na Gambia. Katika sherehe za kufunga mashindano hayo , walihudhuriwa wawakilishi wa Wizara ya Michezo ya Senegal na viongozi wa kidini na maafisa wa kisiasa nchini humo.

Aidha kulikuwa na qiraa ya Qur'ani tukufu kutoka kwa washiriki 10 bora wa mashindano hayo.

Katika hotuba yake, Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Daklar alisema udiplomasia wa Qur'ani ni moja ya misingi muhimuwa kituo cha utamaduni cha Iran. Aidha alitoa wito kwa Waislamu kushikamana na Qur'ani ili waweze kustawi.

Washindi katika mashindano hayo wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya kimatiafa ya Qur'ani ya Misri, Libya, Kuwait, Iran na Saudi Arabia.

3509268

captcha