
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoyatoa wakati
alipoonana na waendeshaji wa "Kongamano la Mashahidi Wanamichezo Nchini
Iran" mkutano ambao ulifanyika tarehe 11 Januari 2016, yamesambazwa Jumanne
asubuhi katika kongamano lenye maudhui hiyo lililofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Uwanja wa Michezo wa Azadi, jijini Tehran.
Katika
mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei alipongeza ubunifu wa kuvutia wa
kuwaenzi mashahidi wanamichezo nchini Iran na kusisitiza kuwa: Ni jambo
la lazima kuifanya jamii nchnii ielewe ni kiasi gani watu wa kila namna
walivyojitolea muhanga maisha yao katika njia ya dini na Mapinduzi ya
Kiislamu na kwamba watu hao hawakutoka katika tabaka fulani tu la watu,
bali watu wa matabaka yote wameshiriki kwenye jambo hilo adhimu la
kimaanawi.
Amelitaja suala la kuwaenzi mashahidi wanamichezo nchini
kuwa ni kunazitia nguvu nyoyo na kuimarisha fikra ya kimapinduzi na
kuongeza kuwa: Kijana mwanamichezo ni kigezo kwa sehemu kubwa ya vijana
na kwamba maadili, mienendo na mtindo wake wa maisha unaweza kuwa na
taathira kwa vijana na unaweza kuingoza jamii kuelekea kwenye kuthamini
mambo ya kidini, kimaadili na kimaanawi.
Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja neno la lugha ya Kifarsi la "Pahlevan"
kuwa ni lakabu yenye ubora wa namna yake katika fasihi ya jadi na ya
kitaifa kwa Iran na huku akiwaenzi wanamichezo ambao wanafanya vitendo
vizuri katika maeneo yao ya michezo amesisitiza kuwa: Fakhari kubwa
zaidi inayopindukia fakhari ya kusomwa wimbo wa taifa au kupandishwa juu
bendera ya nchi baada ya kupatikana ubingwa katika medani fulani ya
michezo, ni kitendo cha mwanamichezo ambaye anakataa kupigana mweleka na
mpinzani Mzayuni au yule mwanamichezo wa kike ambaye anasimama juu ya
jukwaa la ubingwa akiwa amevaa "chadoro" au hijabu kamili ya Kiislamu.
Ayatullah
Udhma Khamenei ameyataja mambo hayo kuwa ni mithili ya kwenda kwenye
medani ya vita na kuonesha moyo mkubwa wa kimapambano wa Muirani
Muislamu katika medani tofauti. Ameongeza kuwa: Vitendo hivyo vinaonesha
utambulisho wa taifa na ni jambo linaloimarisha dhati yao na hiyo ni
silaha madhubuti kwao iliyo imara mithili ya chuma cha pua ambayo
inawasaidia kusimama kidete na kutozubaishwa wala kushindwa na wimbi la
mawazo chapwa na hisia danganyifu, na kwa kweli inabidi kuzifanya medani
zote za michezo zielekee upande huo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
ya Kiislamu amesema kuwa, ni jambo zuri sana kuwaenzi wanamichezo ambao
wanalinda waziwazi matukufu ya kidini katika medani ya michezo.
Ameongeza kuwa: Moja ya kazi ambazo inabidi zifanywe ni kuwaenzi
wanamichezo ambao wanaanza michezo yao kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu
na wale wanamichezo ambao wanapomaliza pambano wanaporomoka chini
kusujudu kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Amesema, jambo hilo
ni nembo ya utambulisho na ndiyo shakhsia ya Iran ya Kiislamu na
kusisitizia udharura wa kutiwa nguvu suala hilo na kuelezea matumaini
yake kuwa, kadiri siku zitakavyosonga mbele, ndivyo maeneo na medani za
michezo zitakavyokuwa safi zaidi na zenye uwazi zaidi.
3472219