IQNA

Barabara yenye jina la kinara wa ISIS mjini Riyadh, Saudia

15:28 - February 03, 2016
Habari ID: 3470112
Wananchi wa Saudi Arabia wameutaka ukoo tawala wa Aal-Saud kubadilisha jina la barabara moja mjini Riyadh iliyopachikwa jina la kinara wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS au Daesh, Abu Bakr al-Baghdadi.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wakiongozwa na mwalimu Ahmad al-Hakami wametuma ujumbe katika ukurasa rasmi wa mtandao wa Watsapp wa Manispaa ya Riyadh wakiitaka ibadilishe jina hilo.

Jarida la mtandaoni la Saudia la Sabq limeandika kuwa, baada ya kuongezeka malalamiko hayo ya wananchi, Manispaa ya Riyadh katika ukurasa wake huo wa Watsapp imesema kuwa, pendekezo hilo limefikishwa kwa mamlaka husika.

Wasaudia wengi wamekuwa wakitoa wito mara kwa mara wa kutaka barabara hiyo inayoitwa Abu Bakr al-Baghdadi, ambayo ipo katika wilaya ya kaskazini mwa mji mkuu Riyadh, ibadilishiwe jina.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh linaloongozwa na Abu Bakr al-Baghdadi limekuwa likifanya mauaji na jinai za kutisha dhidi ya watu wa dini, madhehebu na jamii zote wakiwemo Waislamu wa Kishia, na Kisuni, Wakurdi na Wakristo hususan katika nchi za Iraq na Syria.

3472622

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha