IQNA

Kinara wa magaidi wa ISIS atoroka Mosul kwa msaada wa Marekani

10:05 - March 10, 2017
Habari ID: 3470887
IQNA: Kinara wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh ametoroka mji wa Mosul, Iraq kwa msaada wa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo.

Hayo yamedokezwa na Jawad Al Talibawi kamanda wa Wapiganaji wa vikosi vya kujitolea vya wananchi Iraq maarufu kama Al-Hashd Al-Shaabi ambaye ameongeza kuwa, wanajeshi wa Marekani wamemsaidia Al Baghdadi kutoroka na kujificha katika eneo la Al-Qayrawan. Amesema taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa kinara huyo wa ISIS yuko baina ya Al-Qayrawan na eneo la Al Hadhr yapata kilomita 80 kusini mwa Mosul.

Siku ya Jumatano, Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon ilisema kuna uwezekano kuwa Al Bagdadi ameondoka Mosul na kujificha katika maeneo ya jangwani nje ya mji huo.

Siku chache zilizopita, iliripotiwa kuwa al-Baghdadi alitoa  hotuba ya mwisho akikiri kushindwa kundi hilo nchini Iraq na akiwataka wafuasi wake kukimbilia maeneo ya milimani kwa usalama wao au kujiripua.

Ushindi vilioupata vikosi vya jeshi la Iraq katika mji wa Mosul kukiwemo kudhibiti majengo muhimu ya serikali umewapelekea makamanda wa kundi la kigaidi la ISIS kuwataka magaidi waukimbie mji wa Mosul na kuelekea Raqqa nchini Syria. Mji wa Mosul unafahamika kama ngome muhimu na ya mwisho iliyokuwa ikishikiliwa na magaidi wa ISIS nchini Iraq.

Kinara wa magaidi wakufurishaji wa ISIS, Ibrahim al Sammarai, maarufu kama Abu Bakr al-Baghdadi, alikuwa ameutangaza mji wa Mosul kuwa mji mkuu wa kile alichodai kuwa eti ni khilafa.

Magaidi wa ISIS wamekuwa wakiendesha kampeni ya mauaji ya kinyama nchini Iraq na Syria tokea mwaka 2014. Kundi hilo lenye itikadi za Kiwahhabi, ambalo linapata himaya ya baadhi ya nchi za Magharibi na pia baadhi ya madola ya Kiarabu hasa Saudi Arabia.

3582525
captcha