IQNA

Kongamano la 'Qur'ani, Umaanawi katika Dunia Isiyo na Machafuko'

17:42 - February 25, 2016
Habari ID: 3470160
Kongamano la kitaalamu la 'Qur'ani, Umaanawi katika Dunia Isiyo na Machafuko' limepangwa kufanyika tarehe 16 Machi nchini Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, na litaendelea kwa muda wa siku mbili. Kati ya watakaohutubu katika kikao hicho ni Khushmanesh, Mkuu wa Kituo cha Ustawi na Utafiti wa Qur'ani katika Wizara ya Elimu na Teknolojia Iran na mhadhiri mwingine wa Qur'ani na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Imam Sadiq AS.

Katika kuandaa kongamano hilo, Sayyid Hassan Ismati, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Dakar.

Wamejadili njia za kuandaa kongamano hilo kwa mafanikio ambapo Bw. Ismati amesisitiza kuhusu nafasi muhimu ya Qur'ani katika mahusiano ya kiutamaduni. Amesema kongamano hilo limeitishwa ili kufikia malengo ya Qur'ani Tukufu katika uga wa umoja wa Kiislamu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislamu Dakar amebainisha furaha yake ya kushirikiana na Idara ya Utamaduni ya Iran mjini humo katika kuandaa program za kielimu na Qur'ani. Amebainisha azma ya taasisi yake kushirikiana zaidi na Iran katika utafiti wa Qur'ani Tukufu.

3478227

captcha