IQNA

Iran, mgeni wa heshima katika mjumuiko mkubwa wa Qur’ani Senegal

0:30 - July 27, 2016
Habari ID: 3470477
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imealikwa kama mgeni wa heshima katika Mjumuiko Mkubwa wa 9 wa Qur’ani nchini Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumuiya ya Kitaifa ya Shule na Taasisi za Qur’ani Senegal imeualika ubalozi wa Iran na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini humo katika sherehe iliyopoewa jina la "journée coranique” au Siku ya Qur’ani.

Sherehe hiyo ya kitaifa imepengwa kufanyika Julai 30 chini ya usimamici wa Rais wa Senelga Macky Sall, Malkhlifa wa kieneo na viongozi wa tariqa za Kisufi nchini humo.

Sherehe hiyo inatazamiwa kuwaleta pamoja washiriki 3000 wakiwemo wanazuoni na wasomaji Qur’ani pamoja na raia wa kawaida.

‘Diplomasia ya Qur’ani’ ndio kauli mbio ya sherehe za mwaka huu ambazo zimeandaliwa na Taasisi ya Qur’ani ya Dakar.

Kituo cha Utamaduni cha Iran kimepanga maonyesho ya Qur’ani pembizoni mwa mjumuiko huo ambapo mada kuu katika maonyesho hayo ni, ‘Qura’ni Tukufu Katika Sanaa.”

Senegla ni nchi ya Afrika Magharibi ambapo asilimia 92 ya watu wake wote miluioni 14.5 wa Senegal ni Waislamu.

/3517847

Kishikizo: iqna senegal
captcha