IQNA

Mkutano wa "Wanafunzi Waislamu, Dunia Isiyo na Machafuko" nchini Senegal

16:39 - May 04, 2016
Habari ID: 3470292
Mikutano wa "Wanafunzi Waislamu, Dunia Isiyo na Machafuko" na mwingine wa "Nafasi ya Wasomi wa Utamaduni Katika Ulimwengu wa Kiislamu ili Kufikia Dunia Isiyo na Machafuko" imepangwa kufanyika wiki ijayo nchini Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mikutano hiyo imeandaliwa na idara ya utamaduni wa Ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa Senegal Dakar. Mkuano huo unalenga kusambaza pendekezo la Iran ambalo lilipitishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu "Dunia Isiyo na Misimamo Mikali na Machafuko".

Mfululizo wa vikao hivyo unafanyika kwa ushirikiano na Kamati ya Wanafunzi wa Twariqa ya Qadiriyya katika Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop mjini Dakar na mwakilishi wa Twariqa ya Tijaniya katika katika mji wa Fatick kaskazini mwa Senegal.

Kwa mujibu taarifa hiyo, katika silsila ya vikao vya kiutamaduni kuhusu kuhusu "Dunia Isiyo na Misimamo Mikali na Machafuko" inahudhuriwa na shakhsia wa kiutamaduni, kielimu na wawakilishi wa Twariqa za Kisufi nchini Senegal.

Asilimia 92 ya watu wote milioni14.5 wa Senegal ni Waislamu.

/3494684

captcha