IQNA

Warsha ya Tajweed Kufanyika nchini Senegal

23:17 - July 29, 2016
Habari ID: 3470482
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW, tawi la Senegal, kimepanga warsha maalumu ya misingi ya tajweed na usomaji Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo itaanza Agosti 1 katika Kituo cha Utamaduni cha Iran, Dakar, mji mkuu wa Senegal.

Warsha hiyo imeandaliwa pia kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kitaifa ya Shule na Taasisi za Qur’ani Senegal ambapo waalimi 30 wa Qur’ani watashriki. Warsha hiyo itaendeshwa na Ustadh Majid Zakilu, mtaalamu na qarii wa Qur’ani Tukufu kutoka Iran. Warsha hiyo ya siku sita inatazamiwa kumalizika Agosti 6.

Senegal ni nchi iliyo katika pwani ya Afrika Magharibi na asilimia 92 ya wakaazi wake ni Waislamu. Kwa mujibu wa nyaraka za historia, Uislamu ulifika Senegal katika karne ya 11 Miladia.

3518077

captcha