IQNA

Wananchi wa Iran wanapiga kura katika chaguzi za Bunge na Baraza la Wataalamu

7:31 - February 26, 2016
Habari ID: 3470162
Wananchi wa Iran leo wanapiga kura katika chaguzi mbili muhimu za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge, na Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Iran amesema kuwa maandalizi na taratibu zote za uchaguzi wa kumi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na wa tano Baraza la Wataalamu zimekamilika.

Muhammad Hussein Muqimi amesema kuwa nyezo na vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kupiga kura vimepelekwa mapema katika majimbo yote ya uchaguzi hapa nchini.

Muqimi ameongeza kuwa uchaguzi huo unaanza asubuhi hii saa mbili kamili na utaendelea kwa masaa kumi hadi saa 12 jioni. Amesisitiza kuwa muda huo yumkini ukazidishwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura iwapo italazimu.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu pia amewataka wananchi wote waliotimzia masharti kushiriki kwa wingi na kwa nishati katika zoezi hilo la kidemokrasia ili kuzidisha nguvu ya taifa na rasilimali ya kijamii ya Iran kwa kuonesha umoja na maadili ya Kiislamu.

Waziri Rahmani Fazli ameshiria uelewa na umakini wa taifa la Iran katika kukabiliana na njama za maadui wa kigeni ikiwemo Uingereza na ametoa wito wa wananchi kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo kwa ajili ya maslahi ya kitaifa. Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na tasisi mbalimbali, inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia sabini ya wananchi waliotimiza masharti watashiriki katika zoezi hilo la kupiga kura.

Karibu Wairani milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura katika chaguzi hizo mbili.

Waandishi habari 473 kutoka nchi 29 duniani wapo hapa nchini kwa ajili ya kuripoti matukio ya uchaguzi wa kesho.

Waandishi habari 473 kutoka nchi 29 duniani wapo hapa nchini kwa ajili ya kuripoti matukio ya uchaguzi wa leo.

3478233

captcha