Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Al Tablawi ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani (Quraa) amesema serikali ya Misri inawapuuza quraa (wasomaji) na hufadh (waliohifadhi) Qur'ani na kutowazingatia. Amesema bajeti iliyotengwa kwa ajili ya wanaharakti wa Qur'ani ni duni sana.
Ameongeza kuwa: "Wizara ya Awqaf Misri haijatoa bajeti ya kutosha kwa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani."
Sheikh Tablawi amesema jumuiya hiyo imetoa maombi kadhaa kwa wizara ya awqaf bila mafanikio na kuongeza kuwa jumuiya hiyo na quraa elfu nane wanachama ambao inabidi wasaidiwe ili waweze kuendeleza harakati zao za Qur'ani.