IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun

Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Tablawi aaga dunia

17:48 - May 08, 2020
Habari ID: 3472743
TEHRAN (IQNA)- Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Mahmoud Tablawi ameaga dunia Jumnne akiwa na umri wa miaka 86.

Sheikh Tablawi, ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasomaji Qurani na Waliohifadhi Qur’ani Misri aliaga dunia baada ya kuihudumia Qur’ani kwa muda wa miaka 60.

Msemaji wa Jumuiya ya Wasomaji Qurani na Waliohifadhi Qur’ani Misri ametuma risala za rambi rambi kwa niaba ya wanachama wenzake.

Nayo Dar ul Iftaa ya Misri imetuma salamu za rambi rambi kufuatia kauga dunia qarii huyo mashuhuri wa Qur’ani Tukufu.

Mohamed Mahmoud Tablawi alizaliwa Novemba 14, 1934 katika kijiji cha Met Oqna nchini Misri. Alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri wa miaka mine na kuhitimua akiwa na umri wa miaka 9. Alipata taufiki ya kusafiri katika nchi nyingi duniani akiwa mwakili wa Al-Azhar na Wizara ya Wakfu ya Misri. Halikadhalika aliwahi kuwa jaji katika mashindano mengi ya Qur’ani ya kimataifa.

Qarii huyo amezikwa Alhamisi katika eneo la Al Agouza katika jimbo la Giza magharibi mwa Ukingo wa Mto Nile nchini Misri.

3896800

captcha