IQNA

Mashindano ya Qur'ani yaanza Malaysia

14:35 - May 02, 2016
Habari ID: 3470285
Mashindano ya 58 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yameanza Jumatatu katika mji wa Kuala Lumpur nchini humo.

Mashindano hayo yatakuwa na washiriki 120 kutoka nchi 70 ambao watashindano katika vitengo vya kuhifadhi na kusoma Qur'ani. Halikadhalika mashindano hayo yana jopo la majaji 16 ambao ni wataalamu wa Qur'ani kutoka Lebanon, Qatar, Brunei, Saudi Arabia, Jordan, Indonesia, Misri, Thailand na Malaysia.

Mwakilishi wa Iran katika mashindano hayo katika kitengo cha qiraa ni Seyed Mostafa Hosseini ambaye atasoma siku ya Jumatano.

Mashindano ya 58 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia mwaka hii yanafanyika chini ya kualimbiu ya "Kongamano la Kimataifa la Qiraa na Hifdhi ya Qur'ani Tukufu."

Kuna ujumbe wa ngazi za juu wa wasomi wa Qur'ani na waandishi habari kutoka mashirika kadhaa ya habari ambao watakuwa na jukumu la kutangaza tukio hilo la kimataifa la Qur'ani.

3493941

Kishikizo: iqna
captcha