Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mtihani huo ulifanyika Jumatano katika Msikiti wa Jamia wa Baiturrahman mjini Banda Aceh.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Aceh, Ridwan Hadi amesema mtihani huo ulikuwa moja ya masharti ambayo wanaotaka kugombea ugavana na unaibu gavana wanapaswa kutimiza.
"Sharti la kusoma Qur'ani Tukufu ni la Aceh peke yake na wanaotaka kuwania iwapo hawawezi kusoma Qur'ani basi hawataidhinishwa kushiriki katika uchaguzI," amesema Hadi.
Tume Huru ya Uchaguzi ya Aceh imesema mbali na kubaini uwezo wa kusoma Qur'ani wa wagombea, tume hiyo pia katika siku za usoni itachunguza uwezo wa wagombea kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu.
Baada ya mtihani, Ridwan amewakumbusha wagombea wote wa Ugavana kuwa wanapaswa kuchangia mazingira ya amani wakati wa uchaguzi wa eneo la Aceh ambalo linahesabiwa kuwa kitovu cha Uislamu nchini Indonesia.
Indonesia ni nchi iliyo kusini Mashariki mwa Asia na ina idadi ya watu milioni 249 ambapo milioni 202 ni Waislamu na hivyo kuifanya kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.
3461048