Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Hossein Jaberi Ansari ametoa tamko hilo kupitia taarifa yake siku ya Jumamosi baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kutoa taarifa ya ugaidi duniani ambapo ilidai kuwa eti Iran ni muungaji mkono ugaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Wakati Marekani inaopunga mkono magaidi wa ISIS na makundi mengine ya kigaidi katika eneo, ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo iliyo mstari wa mbele wa kupambana na ugaidi Iraq na Syria."
Ameongeza kuwa, Iran daima imekuwa tayari kushirikiana na serikali zingine pamoja na mashirika ya kimataifa katika vita dhidi ya ugaidi duniani.
Jabaeri Ansari aidha ameikosoa vikali Marekani kwa kutoa taarifa za kujibunia zenye lengo za kupotosha ukweli.
Amesisitiza kuwa, Marekani inatumia sera za kinafiki na kindumakuwili katika kukabiliana na ugaidi kwani Washington ni mmoja kati ya wahusika wakuu wa ugaidi katika eneo na duniani.
Ameongeza kuwa, Marekani inatumia ugaidi kwa maslahi yake na kupuuza jinai zinazotekelezwa na magaidi dhidi ya raia jambo ambalo limepelekea kuwa vigumu vita dhidi ya ugaidi.