IQNA

Polisi nchini Ghana wajengewa msikiti

1:31 - June 07, 2016
Habari ID: 3470365
Serikali ya Ghana imewajengea polisi nchini humo msikiti wao maalumu kwa ajili ya kufanya ibada na kujifunza Kiislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Msikiti huo wenye uwezo wa kubeba watu 1000 umejengwa mjini Accra, mji mkuu wa nchi hiyo, huku ukiwa na ukumbi wa maktaba, ofisi kadhaa na eneo la kuegesha magari. Naibu kamanda wa polisi nchini Ghana ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la nchi hiyo la Daily Graphic na kuongeza kuwa, lengo la kujengwa nyumba hiyo ya ibada kwa ajili ya maafisa wa polisi Waislamu ni kudhamini ustawi na kuinua umaanawi wa kiroho wa polisi . Kadhalika amesema kuwa, umuhimu wa kuhifadhiwa moyo wa kiroho na kiakhlaqi kwa polisi ya nchi hiyo ni kuwafanya polisi hao waweze kuwa na moyo wa kuwapenda wananchi na kusisitiza kuwa serikali inaliona suala hilo kuwa lenye umuhimu kwa polisi wake. Akiashiria sababu ya kuwekwa maktaba ndani ya msikiti huo amesema kuwa, serikali ya Accra inalipa umuhimu suala la polisi kusoma na kufanya uchunguzi wa kidini si tu kwa polisi Waislamu, bali hata kwa wafuasi wa dini nyingine na kwamba hilo litasaidi kuimarisha umoja na amani katika jamii. Serikali ya nchi hiyo imechukua uamzi wa kujenga msikiti huo muhimu kwa polisi, katika hali ambayo Ghana ni nchi yenye idadi kubwa ya Wakristo, suala ambalo limetajwa na jamii ya nchi hiyo kuwa lenye taathira chanya ya kudumisha umoja na upendo baina ya raia wake.

Kishikizo: ghana polisi msikiti iqna
captcha