IQNA

Mkutano wa Waislamu wa Ghana:

Kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu kupitia umoja wa Waislamu

21:55 - October 31, 2024
Habari ID: 3479677
IQNA – Mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana amesema kuwa: “kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu kunahitaji hatua za maana katika suala la umoja wa makundi ya Kiislamu.”

Kwa mujibu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mawasiliano wa Kiislamu (ICRO), Amir Heshmati, Mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana amesema hayo katika Kongamano la Nne la kila Mwaka la Taifa la Waislamu Ghana ambapo amesisitiza kuwa iwapo Waislamu watasimama kidete basi "hatua zinazofaa kuhusu masuala ya pamoja" zitafikiwa.
Ameelezea matumaini kwamba mkutano wa Waislamu wa Ghana utasaidia kuongeza juhudi katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Heshmati ameutaja umoja na kufanya kazi pamoja kuwa ni hakikisho la mustakbali mwema kwa jamii ya siku zijazo na akaongeza kuwa: “Kwa bahati nzuri, kwa hekima ya wanazuoni wa Kiislamu Ghana, mazingira yenye thamani na uaminifu yameundwa kwa ajili ya harakati ya Waislamu nchini humo.

”Katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Waislamu Ghana, zaidi ya washiriki 300 wakiwemo watu mashuhuri wa kitaifa, Sheikh Usman Nuhu Sharbuto, Imamu wa Waislamu wa Ghana, John Dramani Mahama, rais wa zamani wa nchi, Hujjatul Islam Sheikh Abu Bakr Ahmed Kamaluddin, Imamu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Ghana, Sheikh Omar Ibrahim, Imamu wa Jamii ya Ahul Sunnah, Sheikh Abdul Wadud Harun, Imam wa Twariqa ya Tijjaniyya, Imam Muhammad bin Saleh na wabunge wengine, viongozi wa makabila, viongozi na vyama vya siasa na wanawake wa Kiislamu wenye ushawishi pia walishiriki katika hafla hiyo.
4245322

Kishikizo: waislamu ghana
captcha