IQNA

Uzinduzi wa Msikiti wa Al-Mustafa na Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani katika mji mkuu wa Ghana

16:57 - May 07, 2025
Habari ID: 3480650
IQNA – Msikiti mpya umezinduliwa katika mji mkuu wa Ghana kwa ufadhili wa Taasisi ya Misaada ya Qatar .

Msikiti huo unaojulikana kama Masjid Al-Mustafa, uko kando ya Hospitali ya Kijeshi Na. 37 huko Accra na unahudumu kama alama muhimu ya Kiislamu na ni makao ya Kituo cha Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani, hivyo kuimarisha nafasi yake kama taa ya imani katika mji mkuu.

Sherehe ya ufunguzi ilihudhuriwa na wageni mashuhuri, wakiwemo Mkuu wa Jeshi la Wanamaji, Admeri Issa Adam Yakubu, ambaye alikuwa mgeni wa heshima, pamoja na Kamanda wa Hospitali ya Kijeshi Na. 37 Kanali Prosper Aibor, Mkurugenzi wa Masuala ya Kidini Brigedia Jenerali Kumi Wood, na Mwakilishi wa Shirika la One Ummah nchini Ghana, Tariq Marabi.

Brigedia Jenerali Kumi Wood alielezea furaha yake kwa kufunguliwa kwa msikiti huo, akisisitiza umuhimu wake kwa wanajeshi na raia.

Alisisitiza kuwa ilikuwa ni heshima kubwa kushiriki katika uzinduzi wa jengo hili la kidini, ambalo linatoa nafasi muhimu ya ibada kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Kijeshi Na. 37, maafisa wa ulinzi, wafanyakazi wa kiraia, familia zao, na wananchi wanaotembelea.

Makamu Admirali Yakubu alisisitiza jukumu muhimu la msikiti huo mpya, akieleza umuhimu wake kama kimbilio la kiroho kwa wanajeshi na familia zao.

Alielezea msikiti huo kama taa ya kisasa ya imani, inayowakilisha utofauti na umoja ndani ya jamii yao.

Kwa upande wake, Marabi, mwakilishi wa Shirika la One Ummah nchini Ghana na msemaji wa wafadhili binafsi waliochangia ujenzi wa upya wa msikiti huo, alitoa shukrani zake kwa uongozi wa kijeshi kwa kushirikiana na Qatar Charity katika ujenzi huo.

Marabi alishukuru kila mtu aliyehusika kufanikisha mradi huo na alisisitiza wajibu wa kurudisha kwa jamii ya Ghana, ambayo imewapa fursa za kukua na kuendeleza. Alikiri uaminifu na sifa nzuri ya Taasisi ya Qatar Charity nchini Ghana, jambo lililowahamasisha wafadhili kuunga mkono mradi huu wa maana.

3492965

Kishikizo: ghana waislamu
captcha