IQNA

Turathi za Kiislamu

Msikiti wa Larabanga wa Ghana; Kivutio cha Kiislamu Afrika Magharibi

19:34 - July 30, 2023
Habari ID: 3477361
ACCRA (IQNA) - Msikiti wa Larabanga ni mahali pa ibada ya Waislamu nchini Ghana ambao ulijengwa karne ya 15 Miladia.

Uko katika kijiji cha Larabanga, ni msikiti wa kwanza nchini Ghana uliojengwa kwa mtindo wa usanifu wa Sudan.

Pia ni moja ya misikiti kongwe iliyosalia katika eneo la Afrika Magharibi na wengine wameupa lakabu ya "Makka ya Afrika Magharibi".

Inasimuliwa kwamba mfanyabiashara Mwislamu aitwaye Ayub aliota ndoto ambapo aliamriwa kujenga msikiti.

Alifanya hivyo mwaka 1421 Miladia na baada ya kifo chake, alizikwa karibu na mti wa Mbuyu katika msikiti ambao bado upo.

Wenyeji hutumia majani na shina la mti huu wa mbuyu kwa uponyaji wa magonjwa.

Kuna Msahafu wa kale unaohifadhiwa msikitin hapo  ambao ulizawadiwa kwa imamu wa msikiti , Yidan Barimah Bramah mnamo 1650.

Msikiti huo uliojengwa kwa mbinu ya  adobe ya Afrika Magharibi, una minara miwili mirefu yenye umbo la piramidi, mmoja wa mihrab.

Tangu kujengwa kwake mnamo 1421, imekarabatiwa na kukarabatiwa mara kadhaa.

Shirika lisilo la kiserikali la World Monuments Fund (WMF) linalojihusisha na kuhifadhi na kulinda maeneo ya kale na ya kihistoria yaliyo hatarini kutoweka duniani kote, limechangia pakubwa katika juhudi za hivi karibuni za ukarabati wa msikiti huo.

Ghana’s Larabanga Mosque; Mecca of West Africa

Ghana’s Larabanga Mosque; Mecca of West Africa

Ghana’s Larabanga Mosque; Mecca of West Africa

Ghana’s Larabanga Mosque; Mecca of West Africa

 

4152435

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ghana msikiti
captcha